Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:50

Kiongozi wa Kihindu auwawa Bangladesh


Kiongozi wa kidini ya Hindu aliuwawa kwa kile polisi wanachohofia kuwa mashambulizi yakupangwa dhidi ya Wahindu katika nchi yenye Waislamu wengi ya Bangladesh.

Kiongozi huyo aliyekuwa katika wadhifa huo kwa miaka saba, Ananda Gopal Ganguly, alikutwa amefariki dunia nyumbani kwake katika kijiji cha Noldanga saa kadhaa baada ya kupotea alipokuwa akielekea katika sala ya asubuhi.

Mwili wake uliopatikana umeonyesha alama sawa na Wahindu na Wakristo waliokamatwa na kuwawa na wanamgambo wa kislamu.

Zaidi ya watu 40 wamesha uwawa katika mashambulizi kama hayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na ghasia zimeongezeka katika miezi kadhaa iliyopita.

XS
SM
MD
LG