Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:37

Maafisa wa Afghanistan wapambana na kundi la Taliban


moshi ukitoka kwenye jengobaada ya shambulizi la Taliban katika jimbo la Helmand .
moshi ukitoka kwenye jengobaada ya shambulizi la Taliban katika jimbo la Helmand .

Shambulizi la katika wilaya ya Girishk lililenga makao makuu ya polisi na ofisi za Idara ya Upelelezi huko Afghanistan

Maafisa kwenye jimbo la mbali la kusini mwa Afghanistan la Helmand wanasema kundi la wapiganaji wa Taliban wasiopungua 10 wenye silaha nzito wamefanya mashambulizi yaliyopangwa kufanyika kwa wakati mmoja na kuzusha mapambano ya bunduki na vikosi vya usalama.

Shambulizi la mapema Jumanne katika wilaya ya Girishk lililenga makao makuu ya polisi na ofisi za Idara ya Upelelezi huko Afghanistan.

Mashambulio hayo yamesababisha kifo cha polisi mmoja na wengine kujeruhiwa.

XS
SM
MD
LG