Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:30

Shambulizi la kuvizia lafanyika DRC


Washambuliaji waliwaua walinzi watatu na mjumbe wa msafara wao katika shambulio la kuvizia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Alhamisi asubuhi, taasisi ya uhifadhi wa mazingira ya Congo (ICCN) imesema.

Watu hao walishambulia wakati msafara huo uliokuwa ukisindikizwa na walinzi wa ICCN kutoka kijiji cha Kivandya karibu na hifadhi ya Virunga, ambayo ni makazi ya nusu ya idadi ya sokwe wa milimani walio hatarini kutoweka na eneo la mashambulizi ya mara kwa mara ya wanamgambo.

Mwathiriwa wa nne alikuwa mmoja wa wafanyikazi wa kiufundi waliokuwa wakisafiri katika msafara huo ambao walikuwa wakitekeleza mradi wa kusaidia jamii zinazozunguka Virunga, ICCN ilisema katika taarifa.

Watu wengine sita walijeruhiwa, ilisema taarifa.

XS
SM
MD
LG