Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 21:08

Shambulizi la Israel lauwa 6 Gaza


Shambulizi la anga ya Israel, kwenye nyumba moja katika mji wa kusini mwa Gaza limesababisha vifo vya watu tisa, sita kati yao wakiwa watoto, maafisa wa hospitali wamesema Jumamosi, wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake ya takriban miezi saba katika eneo lililozingirwa la Palestina.

Vita vya Israel dhidi ya kundi la wanamgambo wa Hamas vimesababisha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika eneo ambalo tayari ni tete la Mashariki ya Kati.

Mashambulizi hayo yalikwenda kwenye jengo la makazi katika kitongoji cha Tel Sultan magharibi mwa mji wa Rafah, kwa mujibu wa walinzi wa kiraia wa Gaza.

Miili ya watoto hao sita, wanawake wawili na mwanamme mmoja ilipelekwa katika hospitali ya Rafah Abu Yousef al-Najjar, taarifa za hospitali hiyo zilionyesha.

Hospitalini, jamaa walilia na kuikumbatia miili ya watoto hao ikiwa imefungwa sanda nyeupe huku wengine wakiwafariji.

Forum

XS
SM
MD
LG