Maafisa wa usalama wa Iraq wanasema magaidi wa Islamic State wameua karibu watu 35 na kujeruhi wengine kadhaa Alhamisi jioni katika shambulizi kwenye sehemu takatifu ya washiha kaskazini mwa Baghdad.
Shambulizi katika sehemu hiyo inayojulikana kama Sayyid Mohammed inajumuisha mabomu kadhaa ya kujitoa muhanga, bunduki, na maguruneti, limetokea siku kadhaa baada ya mamia ya watu kuuwawa na kujeruhiwa katika shambulizi katika sehemu ya biashara yenye mkusanyiko mkubwa mjini Baghdad, shambulizi baya kuliko katika historia ya Iraq.