Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:30

Milipuko ya mabomu yaua watu 22 nchini Iraq


Mabomu mawili ya kwenye gari yameuwa takriban watu 22 asubuhi ya leo kwenye mji mkuu wa Iraq.

Bomu la kwanza limelenga barabara yenye harakati nyingi za biashara mashariki mwa Badhdad na kuuwa raiya 15 huku wengine 35 wakiwa wamejeruhiwa.

Bomu la pili limetokea kwenye kituo cha mabasi karibu na mojawapo ya vituo vikubwa vya kijeshi nchini kaskazini mwa mji huo na kuuwa takriban watu 12 huku wengine 28 wakijeruhiwa.

Hakuna aliedai kuhusika na mashambulizi hayo lakini kundi la Islamic State limekua likidai kuhusika na mashambulizi katika miezi ya karibuni.

Msemaji wa kijeshi mjini Baghdad amesema mashambulizi mjini humo hayajapunguka licha ya kampeni ya mashambulizi kutoka kwa serikali dhidi ya wanamgambo wa Islamic State mjini Fallujah.

XS
SM
MD
LG