Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 05:42

Shambulizi la droni lauwa zaidi ya watu 40 Sudan


Moto kutokana na shambulizi la anga mjini Khartoum. Picha ya maktaba.
Moto kutokana na shambulizi la anga mjini Khartoum. Picha ya maktaba.

Shambulizi la drone Jumapili kwenye soko moja la wazi kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khratoum, limeua takriban watu 43, wanaharakati na makundi ya kimatibabu wamesema, wakati jeshi la serikali na kundi la kijeshi lenye silaha la RSF wakiendelea kupigania udhibiti wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, wengine 55 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo kwenye kitongoji cha May ambako wapiganaji wengi kutoka RSF walikuwa wametumwa, shirika la madaktari wa Sudan limesema.

Waliojeruhiwa wamepelekwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Bashair kwa matibabu. Kundi la wanaharakati la Resistance Committee ambalo hupanga misaada ya kibinadamu limeweka video kwenye mitandao ya kijamii, ikionyesha miili ya watu waliofungwa kwa mashuka meupe, kwenye uwanja uliopo nje ya hospitali.

Sudan imekuwa kwenye ghasia tangu Aprili baada ya mapigano kuzuka kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na vikosi vya Rapid Support Forces, RSF, vinavyoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Forum

XS
SM
MD
LG