Msemaji wa kundi la Al-Shabaab Somalia Sheikh Abdiasis Abu Musab anaripotiwa kukiri kutokea shambulizi la anga la Marekani katika kambi yake iitwayo Raso kaskazini mwa Mogadishu .
Lakini aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba idadi ya majeruhi iliyotolewa jumatatu ya kuuliwa watu 150 kutokana na shambulizi hilo la Jumamosi ni uwongo kwani anasema ni idadi kubwa kuliko waliofariki.
Msemaji wa White house, Josh Earnest, alithibitisha jana kwamba kulikuwa na shambulizi la anga huko kaskazini ya Mogadishu.
Pentagon imeeleza kwamba ndege zote zisizo na rubani na zilizo na rubani zilitumika kwenye shambulizi hilo kwenye kambi kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia. Ilieleza katika taarifa yake kwamba walitumia taarifa za kijasusi na walikuwa wakifuatilia shughuli katika kambi hiyo kwa wiki kadhaa.