Shambulio la anga la Marekani limemuua kiongozi wa kundi la Islamic State mashariki mwa Syia, kamandi ya jeshi la Marekani imesema Jumapili. Taarifa ya CENTCOM imesema shambulizi la anga lililomuua Usamah al-Muhajir lilifanywa Ijumaa.
Tumeweka wazi kwamba bado tuna nia ya dhati kulishinda kundi la ISIS katika eneo lote, alisema Jenerali Michael “Erik” Kurilla, kamanda wa kamandi kuu ya Marekani. ISIS bado ni tishio, sio tu kwa eneo hilo bali hata Zaidi ya hapo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa operesheni dhidi ya IS, pamoja na vikosi washirika nchini Iraq na Syria, zitaendelea kufikia kushindwa kwa kundi hilo. CENTCOM pia imesema Jumapili kuwa hakuna dalili zozote kwamba raia yeyote aliuawa katika shambulio la anga la Ijumaa.
Hata hivyo, vikosi vya muungano vilitathmini ripoti za raia aliyejeruhiwa. Shambulizi la Ijumaa dhidi ya IS lilifanywa na ndege zisizotumia rubani MQ-9s ambayo ilisumbuliwa na ndege za Russia katika mapabano ambayo yalidumu kwa karibu saa mbili, CENTCOM ilisema katika taarifa.
Forum