Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:52

Shambulizi Kanisani Mombasa lauwa wanne


Polisi wa Kenya ndani ya Kanisa lililoshambuliwa Mombasa, Machi 23, 2014.
Polisi wa Kenya ndani ya Kanisa lililoshambuliwa Mombasa, Machi 23, 2014.

Mashahidi walisema Biblia zilizokuwa na damu pamoja na viti vilivyoangushwa vilitapakazwa kote kwenye sakafu ya Kanisa hilo liitwalo Joy in Jesus lililoko mjini Mombasa.

Watu waliokuwa na bunduki waliingia katika Kanisa moja la pwani ya Kenya leo Jumapili na kushambulia waumini na kuuwa wawili miongoni mwao na kujeruhi wengine wengi.

Vyombo vya habari vya Kenya vinaripoti kuwa waumini wengine wawili wamefariki kutokana na majeraha. Mashahidi walisema Biblia zilizokuwa na damu pamoja na viti vilivyoangushwa vilitapakazwa kote kwenye sakafu ya Kanisa hilo liitwalo Joy in Jesus lililoko mjini Mombasa.

Haikubainika mara moja ni nani waliotekeleza shambulizi hilo lenye maafa, lakini kundi lenye ushirika na al-Qaida la wanamgambo wa Somalia, Al-Shabab na wafuasi wake, limelaumiwa katika siku za nyuma kwa mashambulizi kama hayo.
XS
SM
MD
LG