Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:21

Serikali yafukuza bodi ya shirikisho la kandanda Misri


Serikali yafukuza bodi ya shirikisho la kandanda Misri
Serikali yafukuza bodi ya shirikisho la kandanda Misri

Serikali imewafukuza wanachama wa bodi kuu ya shirikisho la kandanda misri na kumsitisha kazi gavana wa Port Said.

Waziri Mkuu aliyeteuliwa na baraza la kijeshi la Misri, Kamal al-Ganzuri amesema serikali iliamua wakati wa kikao cha dharuracha bunge kuwafukuza kazi wakuu wa Shirikisho la Kandanda la Misri na kuwasitisha kazi gavana wa mji wa kaskazini wa Port Said na wakuu wa usalama kutokana na jinsi walivyoshugulikia ghasia hizo.

Ghasia hizo baada ya mchezo wa kandanda zilizosababisha vifo vya watu 74 na mamia kujeruhiwa zinasemekana kuwa mbaya kabisa katika historia ya michezo nchini humo.

Kufuatia ghasia hizo maelfu ya wakazi wa Cairo na Port Said waliandamana Alhamisi kulaani jinsi vikosi vya usalama vilivyosimama na kuwangalia mamia ya mashabiki wa timu ya mji wa Port Said ya Al-Masry walipowashambulia uwanjani wageni wao kutoka Cairo, Al-Ahly.

Marshali Mohammed Tantawi
Marshali Mohammed Tantawi

Mkuu wa baraza la kijeshi la Misri Marshali Mohamed Tantawi, ametangaza siku tatu ya maombolezi ya kitaifa na kuapa kuwasaka wahusika. Polisi wamewakamata watuhumiwa 47.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Katibu Mkuu wa wa Shirikisho la Kandanda Afrika Mashariki na Kati - CECAFA, Nicholas Musonyi amesema, “sisi kama CECAFA tumesikitika sana kwa sababu jambo kama hilo kutokea nchini Egypt, ni jambo ambalo limeleta aibu sana katika soka barani Afrika”

Anasisitiza kwamba ni lazima Shirikisho la Kandanda liweke usalama kamili katika michezo, kwani watu wana kwenda kijifurahisha kutizama soka lakini usalama ni muhimu zaidi, na hivyo kuzuka ghasia Misri makao makuu ya CAF ni jambo lisilokubalika.

Akizungumzia michuano ya kombe la Afrika inayoendelea huko Gabon na Equatorial Guinea, Bw Musonyi anasema kandanda imebadilika na hakuna tena timu ndogo na timu kubwa.

Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA, Sepp Blatter, ameiandikia barua Shirikisho la Kandanda la Misri kutaka maelezo kamili ya maafa hayo na kueleza kuwa ni "siku ya kiza kwa kandanda".

XS
SM
MD
LG