Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 20, 2025 Local time: 22:42

Serikali ya Tshisekedi yazindua program za maendeleo katika wilaya 145


Serikali ya Rais Felix Tshisekedi imezindua program maalumu kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika wilaya 145 katika mikoa mbalimbali kwa kukuza shughuli za maendeleo.(Malivika).
Serikali ya Rais Felix Tshisekedi imezindua program maalumu kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika wilaya 145 katika mikoa mbalimbali kwa kukuza shughuli za maendeleo.(Malivika).

Serikali ya Rais Felix Tshisekedi imezindua program maalumu  kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika wilaya 145 katika mikoa mbalimbali kwa kukuza shughuli za maendeleo.

Mpango maalum wa kusukuma maendeleo ya taifa la Congo umezinduliwa nchini humo katika mikoa mbali mbali ikiwemo Mkoa wa Ituri na Kinshasa baada ya ule wa Kivu kaskazini ambako kumeripotiwa machafuko na ufukara kwa muda mrefu.

Michael Amuli Ramadhani ni kutoka serikali kuu ya Kinshasa akiambatana na Gavana wa Mkoa wa Ituri Luteni Jenerali Jony luboya Nkashama amesema lengo kubwa la mpango huo ni kuweka maendeleo kote katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika secta mbali mbali .

Wananchi wa mashariki mwa Congo sehemu inayo shuhudia machafuko kwenye vijiji mara kwa mara wakiwa na shaka lakini wameomba vijana wa wa eneo hilo kuwa wa kwanza kupewa ajira ili kupunguza makundi ya waasi.

Wakati huo huo wanawake wameomba utekelezwaji wa miradi hiyo kwani wameshapata ahadi nyingi kutoka serikali za Congo lakini hazijatimizwa kwa muda mrefu. Mama Elizabet Love Buve mmoja wa watetezi wa wanawake mkoani Ituri akiwa Mji Bunia atafuatilia kuona kama ahadi hiyo itatekelezwa.

Mipango kama hii huwa inaahidiwa na serikali kadhaa ila utekelezwaji wake ukipitia changamoto kadhaa ama kushindikana kabisa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Austere Malivika Goma.

XS
SM
MD
LG