Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:51

Serikali ya Tanzania kuchunguza vibali vya kazi vya wahamiaji


Hati ya kusafiria wageni kutoka nchi moja hadi nyingine
Hati ya kusafiria wageni kutoka nchi moja hadi nyingine

Serikali ya Tanzania imetangaza kuazisha operesheni kali ya kuwasaka wahamiaji haramu ikiwemo wale wanaofanyakazi kinyume na sheria .

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:41 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hatua hiyo iliyotangazwa na wizara ya mambo ya ndani nchini tanzania ni sehemu ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu na kuwawezesha watanzania kupata ajira chache zilizoko ndani ya nchi.

Operesheni hiyo ambayo inafanyika maeneo yote nchini inakuja katika wakati ambapo ripoti zikionesha kuwepo kwa idadi kubwa ya wahamiaji wa kigeni wanaofanyakazi katika maeneo mbalimbali bila vibali rasmi.

Hivi karibuni baadhi ya mawaziri walitembelea katika makampuni kadhaa nakubaini kuwepo kwa wafanyakazi hao ambao baadhi yao walidaiwa kufanyakazi ambazo zinapaswa kufanywa na wazawa.

Akitangaza hatua ya kuanza kwa operesheni hiyo naibu waziri wa mambo ya ndani, Hamad Masauni alisema pia mkakati huo utawalenga wale raia wakigeni waliopewa vibali vya kufanyakazi katika mazingira yenye utata.

XS
SM
MD
LG