Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 21:47

Tanzania yasoma bajeti ya mwaka 2016/17


Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.

Serikali ya Tanzania imewasilisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 yenye kauli mbiu ya kuongeza uzalishaji viwandani ili kupanua fursa za ajira nchini huku bajeti hiyo ikielekezwa zaidi kwenye miradi ya maendeleo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Makadirio ya bajeti hiyo ya takribani shilingi za kitanzania Trilioni 29.5 iliyowasilishwa bungeni mjini Dodoma na waziri wa fedha na mipango, Dk. Philipo Mpango pia imejikita katika kutatua kero za wananchi ikiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ambapo serikali imetenga takribani shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kuanzisha mahakama ya mafisadi.

Aidha kwa mujibu wa Dk Mpango serikali imekusudia kuwasilisha kwa hati ya dharura katika kikao hiki cha bunge marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma ili kurudisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma katika kuhakikisha zinatumika ipasavyo katika miradi ya maendeleo . Asilima 40 ya bajeti ya mwaka 2016/17 inakwenda kwenye miradi ya maendeleo.

Akizungumzia kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini ,waziri wa fedha Dr. Mpango alisema ahadi ya Rais John Magufuli ya kupunguza kodi katika mishahara kutoka asilimia 11 mpaka asilimia 9 itaanza kutekelezwa rasmi Julai Mosi mwaka huu.

Akizungumzia marekebisho ya mfumo wa kodi nchini Dr. Mpango alisema serikali imefanya marekebisho kadhaa kwenye kodi ya ongezeko la thamani VAT kwa ajili ya kuongeza mapato na ukusanyaji wa kodi.

Serikali pia imeongeza ushuru katika bidhaa mbalimbali ikiwemo vinywaji baridi, mvinyo, bia na kodi ya usajili na uhamisho wa umiliki wa magari huku pia ikiondoa msamaha wa kodi ya mapato kwenye malipo ya kiinua mgongo kwa wabunge yanayofanywa kila baada ya miaka mitano.

Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.Katika hatua nyingine katika bajeti hii ya mwaka 2016/17 serikali imesitisha misamaha ya kodi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kupitia kwenye migahawa na maduka maalum ambapo sasa itatoa posho ya nyongeza katika posho ya chakula ili kudhibiti uvujaji wa mapato uliokuwa unafanywa kwenye msamaha huo

Kama walivyokubaliana wabunge wote wa kambi ya upinzani bungeni walitoka nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya naibu spika wa bunge Dr. Tulia Ackson kuingia tayari kuanza kusomwa bajeti ya serikali wakiendeleza kampeni yao ya kumsusia vikao vyote atakavyoongoza kwa madai ya kukataa kuburuzwa na naibu spika huyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG