Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 16:50

Serikali ya Sierra Leonne yatetea ongezeko la bei ya mafuta


Serikali ya Sierra Leone yatetea ongezeko la bei ya mafuta

Serikali ya Sierra Leone imetetea ongezeko la bei za bidhaa za mafuta nchini humo. Wiki iliopita ilitangaza kusitisha kutowa ruzuku kwa bidhaa za mafuta wakati ikiongeza bei za mafuta ya taa, dizeli na petrol.

Kulingana na hatua hiyo mpya bei za petrol na dizeli zimepanda kwa senti 67 ambayo ni takriban dola 1.68. Msemaji wa Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, Abdulai Bayraytay alisema kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta ni muhimu ili kuweza kukabiliana na tatizo la kupungua kwa mapato ya serikali baada ya janga la Ebola lililoathiri sekta ya utalii na pia kutokana na kushuka kwa bei ya chuma ya pua inavyochimbwa nchini humo.

Bayraytay alisema kuwa serikali ya APC ilipochukua mamlaka mwaka 2007 nia yake ilikuwa kuimarisha uchumi na kuvutia wawekezaji kutoka nje ili kutengeneza ajira zaidi. Aliongeza kuwa kama hatua ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo serikali imekuwa ikishirikiana na mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia na IMF.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG