Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:57

Serikali ya mpito Somalia imegubikwa na ufisadi-Umoja wa Mataifa


Rais wa Somalia Sheik Sheriff Sheik Ahmed akiongea na maafisa wa serikali baada ya kumwapisha waziri mkuu wake Mohamed Abdullahi Mohamed huko Mogadishu 2010.
Rais wa Somalia Sheik Sheriff Sheik Ahmed akiongea na maafisa wa serikali baada ya kumwapisha waziri mkuu wake Mohamed Abdullahi Mohamed huko Mogadishu 2010.

Ripoti hiyo inaeleza asilimia 70 ya mapato ya serikali hayajafika hazina .

Ripoti moja ya Umoja wa mataifa inaeleza kwamba serikali ya mpito ya Somalia ina ufisadi mkubwa ambao unatawaliwa na kauli maarufu ya kisomali “ Na Mimi Nitapata nini” .

Kundi la ufuatiliaji Somalia na Eritrea la Umoja wa mataifa linaeleza kuwa baadhi ya viongozi wanataka kuteka nyara au kuvuruga utaratibu wa mpito wa kisiasa wa Somalia kwa faida yao binafsi.

Mamlaka ya serikali ya mpito yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Agosti. Na serikali hiyo inadhaminiwa na fedha kwa kiasi kikubwa kutoka Umoja wa mataifa , Marekani na Umoja wa Ulaya.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba asilimia 70 ya mapato ya serikali hayakufikia hazina ya serikali hapo mwaka 2009 na 2010.

XS
SM
MD
LG