Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 22:26

Serikali ya Mali yawapongeza vijana wa kaskazini mwa Mali


Mwanajeshi akitembea na baadhi ya waandamanaji kwenye uwanja wa ndege wa bamako nchini Mali, Machi 29, 2012

ECOWAS wanazungumza na kundi la Tuareg, MNLA na Ansar Dine ili kubuni suluhisho la mgogoro wa kaskazini mwa Mali

Maandamano ya mitaani yanayofanywa na vijana kaskazini mwa Mali wiki hii yalielezea kukasirishwa kwa watu ambao hivi sasa wanaishi katika khofu ya makundi yenye silaha kwa miezi mitatu.

Serikali ya muda ya Mali imepongeza ushujaa na uthabiti wa vijana na kwa mara nyingine serikali imesema itafanya kadri iwezavyo kuondoa kile kinachoitwa magaidi na wahalifu.
Wakazi wa mji wa gao uliopo kaskazini mwa Mali waliingia mitaani siku ya Jumanne baada ya kifo cha afisa mmoja katika eneo ambaye inadaiwa aliuliwa na makundi yenye silaha ambayo hivi sasa yanadhibiti mkoa huo.

Serikali ilitoa taarifa Jumatatno ya kuwapongeza wakazi wa Gao kwa uthabiti wao mkubwa huku wakikabiliwa na manyanyaso, uhalifu na ghasia kubwa zisizo za maana.

Tangu mwishoni mwa mwezi Machi watu wa Gao, Timbuktu na Kidal wanaishi chini ya udhibiti wa waasi wenye silaha wa Tuareg wanaotaka kujitenga na wanamgambo wa ki-Islam. Wakazi wa kaskazini wanaiambia Sauti ya Amerika-VOA wanajihisi kutelekezwa na serikali yao na kwamba licha ya hatari watu wanaonekana kujitokeza wazi wazi kupinga ghasia.

Wapatanishi wa jumuiya ya uchumi ya mataifa ya afrika magharibi -ECOWAS wanazungumza na wawakilishi wa kundi la waasi wanaotaka kujitenga wa Tuareg, National Movement for Liberation of Azawad-MNLA na kundi la wanamgambo wa ki-Islam la Ansar Dine ili kubuni suluhisho. Wakati huo huo viongozi wa kieneo wanaandaa wanajeshi na wanaomba uungaji mkono rasmi wa Umoja wa Mataifa kuingilia kati mgogoro wa kaskazini mwa Mali.

XS
SM
MD
LG