Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 12:54

Serikali ya Mali ipo tayari kufanya mazungumzo na wanamgambo


Mpiganaji wa Tuareg

Waziri mkuu wa mpito wa Mali amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na wanamgambo wa kiislamu ambao uasi wao umefanya eneo kubwa la Mali lisitawalike, lakini ufaransa koloni wl zamani la Mali imepinga wazo hilo.

Moctar Ouane ambae aliteuliwa waziri mkuu wa muda mwezi uliopita kuongoza serekali ya mpito kwa kipindi cha miezi 18 baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18, amesema serekali yake iko tayari kuendelea na mazungumzo na waasi wa kiislamu.

“Maazimio ya mazungumzo ya kitaifa ya pande zote husika, yalieleza wazi umuhimu wa kufanya majadiliano na makundi hayo yenye silaha”, Ouane amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bamako, akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Yves le Drian ambae yuko ziarani nchini Mali.

Lakini Le Drian amesema hakubaliani na fikra hiyo, akieleza kuwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu hayakusaini mkataba wa amani wa mwaka 2015, ambao ulijenga msingi wa kurejesha amani kaskazini mwa Mali.

Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG