Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:52

Serikali ya Kenya yalaumiwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu


Kenya polisi wakifanya doria mbele ya Msikiti wa Musa mjini Mombasa huko Kenya
Kenya polisi wakifanya doria mbele ya Msikiti wa Musa mjini Mombasa huko Kenya

Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini Kenya inawashutumu polisi na majeshi ya usalama kwa ukiukaji mbali mbali ikiwemo mauaji na mateso katika mapambano yanayoendelea dhidi ya ugaidi nchini humo.

Tume ilisema katika ripoti mpya ya Jumanne kwamba ukiukaji wa haki za binadamu umesambaa na uliratibiwa vyema. Wachunguzi wanasema waliambiwa kwenye kesi mbali mbali za washukiwa kwamba walikamatwa kiholela na kuwekwa jela kuanzia saa kadhaa hadi siku nyingi katika hali ya msongamano mkubwa na hali duni.

Polisi wa Kenya na harakati za msako wa magaidi
Polisi wa Kenya na harakati za msako wa magaidi

Kuna shutuma za mateso, kupigwa, kumwagiwa maji na kuchomwa na nyaya za umeme. Baadhi ya washukiwa walining’inizwa kwenye miti na wengine waliachwa wakang’atwe na wadudu.

Ripoti hiyo ilisema watu wenye asili ya kisomali na waislam wamekuwa walengwa wakubwa. Familia zinatafuta taarifa juu ya kupotea kwa jamaa zao na wanapata msaada kidogo kutoka kwa maafisa.

Tume hiyo ilisema huku ikitambua changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Kenya katika kupambana na msimamo mkali na ugaidi, lazima hilo lifanyike kisheria na kulingana na viwango vinavyokubalika ulimwenguni vya haki za binadamu.

Maafisa wa Kenya bado hawajajibu lolote juu ya ripoti hiyo.

XS
SM
MD
LG