Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:14

Serikali ya Israel kuchangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango wa COVAX

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Yair Lapid akihudhuria mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (hayupo pichani) katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington Dc Oktoba 13,2021. Andrew Harnik/Pool REUTERS

Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.

Serikali ya Israel siku ya Jumatano imesema itachangia chanjo milioni 1 za virusi vya corona kwa mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wa COVAX.

Wizara ya Mambo ya Nje ilisema chanjo za AstraZeneca zitahamishwa katika wiki zijazo, uamuzi ambao ulikuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano wa Israeli na nchi za Kiafrika.

Nimefurahi kuwa Israeli inaweza kuchangia na kuwa mshirika katika kutokomeza janga hili ulimwenguni, Waziri wa Mambo ya nje Yair Lapid alisema.

Tangazo hilo lilisema kuwa chanjo hizo zitafikia karibu robo ya nchi za Afrika, ingawa haikutoa orodha. Israel ina uhusiano wa karibu na mataifa kadhaa ya Afrika, yakiwemo Kenya, Uganda na Rwanda. Israel pia ilianzisha uhusiano na Sudan mwaka jana kama sehemu ya mfululizo wa mapatano yaliyosimamiwa na Marekani.

XS
SM
MD
LG