Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 00:05

Serikali ya Guinea yasitisha kampeni za uchaguzi


Kaimu rais wa Guinea Jenerali Sekouba Konate, kushoto, akizungumza na waziri mkuu wa serikali ya mpito Jean Marie Dore.

serikali ya Guinea yapiga marufuku maandamano ya mitaani na kusitisha kampeni za uchaguzi.

Serikali ya Guinea yasitisha kampeni za uchaguzi wa rais .

Serikali ya Guinea imepiga marufuku maandamano ya mitaani na kusitisha kampeni za uchaguzi kufuatia mapambano baina ya wafuasi wa wagombea wawili wa uchaguzi wa rais katika duru yan pili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.

Kaimu waaziri mkuu Jean- Marie Dore anatarajiwa kukutana kwa vikao mbali mbali na wagombea, Cellou Dulein Diallo na Alpha Conde Jumatatu.

Mapambano ya Jumamosi na Jumapili baina ya wafuasi wa wagombea hao wawili yalisababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 50.

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi kubwa la watu ambalo lilikuwa linarusha mawe na kuvamia magari.

Ghasia hizo zimezuka baada ya maafisa wawili wenye vyeo vya juu wa tume ya uchaguzi kutuhumiwa kutoa matokeo ya uongo wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais mwezi Juni.

Diallo ambaye ni waziri mkuu wa zamani alipata ushindi wa asilimia 44 ya kura katika uchaguzi huo. Conde kiongozi mkongwe wa upinzani alichukua nafasi ya pili akiwa na asilimi 18.

XS
SM
MD
LG