Jumapili, mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahmat alitoa wito wa sitisho la mapigano mara moja na bila masharti yoyote, wakati mapigano yakiongezeka katika mkoa wa Tigray, na kuzitaka pande hizo mbili ambazo zinapigana kwa karibu miaka miwili kukubali tena kufanya mazungumzo.
Viongozi wa Tigray Jumapili wamesema wako tayari kutekeleza sitisho la mara moja la uhasama na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuishinikiza serikali ya Ethiopia kufika kwenye meza ya mazungumzo.
Addis Ababa Jumatatu imesema ina dhamira ya kutatua mzozo huo kwa njia ya amani kupitia mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Afrika.