Ghasia za wanamgambo zimekumba eneo kubwa la mashariki lenye utajiri mkubwa wa madini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa miongo miwili licha ya uingiliaji kati wa kijeshi wa ndani na kikanda na juhudi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.
Helikopta iliyokuwa ikiendeshwa na kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO ilishambuliwa siku ya Jumapili baada ya kuruka kutoka mji wa Beni. Mlinda amani wa Afrika Kusini aliuwawa na mwingine mmoja kujeruhiwa.
Si Afrika Kusini wala MONUSCO iliyosema ni nani anaweza kuwa anahusika, wala ni aina gani ya silaha iliyotumika kuilenga helikopta hiyo au ni nini kilisababisha majeruhi.
Serikali ya Kinshasa ilililaumu kundi la M23 katika taarifa yake siku ya Jumatatu. Kundi hilo ambalo lilianzisha mashambulizi makubwa mwaka jana, lilikanusha sgutuma hizo.
Ikiwa na takriban wafanyakazi 18,200, MONUSCO imetumwa mashariki mwa Congo tangu kuchukua nafasi ya operesheni ya awali ya Umoja wa Mataifa mwaka 2010. Jukumu lake ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya Congo kuleta utulivu katika eneo hilo.
Facebook Forum