Serikali ya Burundi imesitisha shughuli za chama kikuu cha upinzani katika nchi hiyo ya Afrika ya kati ikitaja kuwepo na kasoro ambazo wakosoaji walieleza ni jaribio la kuwakandamiza wapinzani kuelekea uchaguzi wa wabunge mwaka 2025.
Hatua hiyo ya wizara ya mambo ya ndani iliyotangazwa katika barua iliyotolewa Jumanne inahatarisha kuzuka kwa machafuko ya kisiasa ambayo yameyakumba mataifa masikini ya Maziwa Makuu katika miaka ya hivi karibuni.
Katika kujibu chama cha National Freedom Council (CNL) kililaani ukiukaji mkubwa wa katiba katika jaribio la kuvuruga na kudhoofisha chama baada ya hatua ya karibuni ya kuchorwa upya mipaka ya wilaya katika uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Wizara hiyo imesema inajibu malalamiko ya viongozi wanane wa CNL walioondolewa madarakani baada ya kumpinga rais wa chama hicho Agathon Rwasa katika mikutano miwili ya chama hicho hivi karibuni.
Forum