Serikali mpya ya muda ya Libya ya waziri mkuu Abdullah al-Thani imeapishwa na bunge la Libya Jumapili katika mji wa mashariki wa Tobruk.
Ushirika wa wanamgambo wa kiislamu ambao unadhibiti mji mkuu Tripoli unakataa kumtambua bwana al-Thani na kuunga mkono serikali yake.
Sherehe za kuapishwa zilikuwa fupi na waziri mkuu al- Thani aliapa kulinda uhuru wa nchi, kutetea usalama wake na kuhesimu katiba na sheria. Aliahidi kutekeleza maslahi ya watu na kutetea misingi na malengo ya mapinduzi ya februari 17.
Baraza la mawaziri la bwana al-Thani lilikuwa dogo, chini ya dazani ya mawaziri. Viongozi wa kisiasa wa Libya wamelikebehi baraza jipya kuwa ni “serikali ya mpito yenye mzozo”.
Ushirika wa wanamgambo wa kiislamu Farj, ambao unadhibiti mji mkuu Tripoli unasema unaunga mkono serikali yake yenyewe ambayo bado haijaapishwa rasmi.
Aqelah salah anayeoongoza bunge linalotambulika kimataifa huko Tobruk aliwaambia wabunge kwamba serikali mpya itafanya kazi kujenga taifa imara kulinda amani na uthabiti, kutetea maslahi ya wananchi na kuhakikisha kuna huduma za umma ikiwemo afya na elimu.
Vituo vya televisheni vya kiarabu vinavyorusha matangazo kwa njia ya satellite vimeripoti viongozi wa kisiasa wamekaribisha mjadala wa kitaifa Jumatatu chini ya usimamizi wa umoja wa mataifa. Haikufahamika haraka, hata hivyo kama makundi yote ya kisiasa yanapanga kuhudhuria.
Ahmed al- Atrash anayefundisha siasa na mahusiano ya kimataifa katika chuo kikuu cha Tripoli ameiambia sauti ya Amerika kwamba ni muhimu kwa makundi yote kuhudhuria mjadala wa kitaifa.