Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 21:19

Serikali Marekani yafanya uchunguzi kuhusu kuchomwa misikiti ya Minneapolis


Wakili Andrew Luger akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari huko Minneapolis, Alhamisi, Mei 4, 2023, kuhusu uchunguzi wa serikali juu ya mtu anayeshukiwa kuchoma misikiti ya Minneapolis hivi karibuni.

Wakili Andrew Luger akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari huko Minneapolis, Alhamisi, Mei 4, 2023, kuhusu uchunguzi wa serikali juu ya mtu anayeshukiwa kuwasha moto misikiti ya Minneapolis wiki iliyopita.

Mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya misikiti huko Minneapolis, katika jimbo la Minnesota, yameongeza wasiwasi wa maimamu wa wamarekani wenye asili ya Kisomali, wasimamizi wa misikiti na wanaharakati wa kijamii kuhusu usalama wa jumuiya zao na shughuli zake.

Moto ulichomwa katika Kituo cha Kiislamu cha Masjid Omar Aprili 23 na Msikiti wa Masjid Al-Rahma Aprili 24, polisi wa Minneapolis walisema. Maeneo hayo yapo karibu karibu.

Jaylani Hussein, mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Mahusiano ya Kimarekani na Kiislamu Minnesota, alikuwa ndani ya Msikiti wa Masjid Al-Rahma wakati mtu alipowasha moto katika ghorofa ya tatu.

“Nilikuwa ndani ya msikiti, nikikutana na Maimamu kuhusu usalama wa watu wake, nilipomsikia mtu akipiga kelele. Kuna moto. Kuna moto”. Hussein aliiambia VOA hivi karibuni. Asante Mungu hakuna aliyejeruhiwa.

Aliongeza kuwa zaidi ya watoto 40 waliokuwa katika huduma ya kulelewa ya msikitini mchana lakini walihamishwa salama.

Hussein anajihusisha na mapambano ya jumuiya ya waislam Marekani dhidi ya mashambulizi ya chuki, lakini alisema hii ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia tukio kama hilo.

XS
SM
MD
LG