Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:38

Serikali ya DRC yakataa kuzungumza na M23


Watoto wakimbizi waliokoseshwa makazi kufuatia mapigano yanayoendelea Kivu kaskazini nchini DRC
Watoto wakimbizi waliokoseshwa makazi kufuatia mapigano yanayoendelea Kivu kaskazini nchini DRC
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC inasema haitakaa mezani kujadiliana na kundi la waasi wa M23 ambao ni wanajeshi wa zamani na ambao hivi sasa wanapigana dhidi ya jeshi la serikali katika jimbo la Kivu kaskazini.

Waziri wa mambo ya nje wa DRC Raymond Tshibanda anasema serikali yake haitaki kundi hilo liwepo wala vitendo vyake kuendelea hivyo basi hakuna kitu chochote cha kuzungumzia nalo wala kutafuta suluhisho.

Tshibanda pia alipuuzilia mbali pendekezo la kuunda “jeshi lisilofungamana na upande wowote” ili kupambana na waasi akisema Congo inapendekeza walinda amani wa Umoja wa Mataifa kuchukua jukumu kubwa zaidi katika mapigano hayo.
Mapigano kati ya serikali na kundi la M23 yamewakosesha makazi maelfu ya watu huko Kivu kaskazini.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano mjini kampala nchini Uganda Tshibanda alirudia madai kwamba Rwanda inahusika kuwasaidia waasi wa M23. Alisema jeshi lolote litakalochaguliwa kupambana na waasi haliwezi kujumuisha wanajeshi wa Rwanda kwa sababu katika maneno yake “Rwanda ni sehemu ya tatizo.”

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwezi Juni ilisema kuna ushahidi wa kutosha kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23. Rwanda inakanusha shutuma hizo. Uganda pia inakanusha shutuma za kusaidia kundi la hilo la waasi.
XS
SM
MD
LG