Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:10

Seneti ya Marekani yapitisha mswada wa sheria kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kupunguza gharama ya dawa


Kiongozi wa walio wengi kwenye Baraza la Seneti Chuck Schumer azungumza na vyombo vya habari, baada ya Seneti kupitisha mswada wa sheria "Inflation Reduction Act of 2022, Agosti 7, 2022. Picha ya Reuters
Kiongozi wa walio wengi kwenye Baraza la Seneti Chuck Schumer azungumza na vyombo vya habari, baada ya Seneti kupitisha mswada wa sheria "Inflation Reduction Act of 2022, Agosti 7, 2022. Picha ya Reuters

Maseneta wa chama cha Democratic Jumapili wamepitisha mswada wa sheria utakaosaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kupunguza gharama za huduma ya afya na kuongeza kodi kwa makampuni yanayopata faida kubwa.

Warepublikan wote wameupinga mswaada huo ambao ulipitishwa kwa kura 51 dhidi ya 50 baada ya makamu rais Kamala Harris kupiga kura yake.

Mswada huo umeidhinishwa baada ya mjadala mrefu wa kufanyia marekebisho vipengele kadhaa ambao ulianza Jumamosi.

Kiongozi wa walio wengi kwenye Seneti mdemocrat Chuck Schumer amesema mswada huo ni mojawapo ya hatua muhimu za kisheria za karne ya 21.

“Baraza la Seneti limeandika historia,” amesema.

Mswada huo umependekeza uwekezaji mkubwa katika historia ya Marekani katika kukabiliana na athari za ongezeko la joto duniani, dola bilioni 370 zitatumiwa katika kuimarisha matumizi ya nishati mbadala, kuhamasisha Wamarekani kununua magari ya umeme na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 40 ifikapo mwaka wa 2030.

Mswada huo kwa mara ya kwanza unairihusu serikali ya Marekani kujadiliana na makampuni ya dawa ili kupunguza gharama za dawa kwa Wamarekani wazee, kuongeza ruzuku ya bima ya afya kwa mamilioni ya watu na kuongeza kodi ya asilimia 15 kwa makampuni yanayopata faida ya zaidi ya dola bilioni 1 ambayo yalikuwa hayalipi chochote.

Mswada huo pia utaongeza mawakala 87,000 wa kutoza kodi ili kuwafuatilia na kuwanasa wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na walaghai wa kodi na kupunguza nakisi ya muda mrefu ya bajeti kwa takriban dola bilioni 300.

XS
SM
MD
LG