Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:57

Seneta Stevens wa Marekani afariki


Seneta Stevens wakati wakiwa bungeni.
Seneta Stevens wakati wakiwa bungeni.

Seneta wa zamani kutoka jimbo la Alaska nchini Marekani Ted Stevens afariki dunia katika ajali ya ndege.

Seneta wa zamani aliyekuwa akiwakilisha jimbo la Alaska nchini Marekani amefariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea huko huko katika jimbo lake Jumanne. Alikuwa na umri wa miaka 86.

Stevens, ambaye alizaliwa katika jimbo la Indiana, aliwakilisha Alaska kwa miaka 40, na kumfanya kuwa Mrepublican aliyekaa katika baraza la seneti kwa muda mrefu kuliko wote.

Alijaribu kuchaguliwa kwa awamu ya saba madarakani mwaka 2008, lakini alishindwa baada kukutwa na hatia ya ulaji rushwa kwa kutotoa ripoti zisizokuwa kweli kuhusiana na zawadi aliyopokea kutoka kwa kampuni moja ya mafuta. Hatia hiyo baadaye ilifutwa kutokana na makosa yaliyofanywa na waendesha mashitaka.

Stevens alinusurika katika ajali ya ndege mwaka 1978 huko Anchorage, Alaska, ajali ambayo ilimwua mke wake kwanza, Ann.

XS
SM
MD
LG