Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 02:10

Senegal yatolewa nje ya kombe la dunia


Washabiki wa Senegal wakiwa na butwaa baada ya timu yao kutolewa na Uingereza huko Al Bayt Stadium, Al Khor, Qatar - December 4, 2022.

Timu ya Senegal -Simba wa Tearnga imetupe nje ya kombe la dunia baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uingereza katika uwanja wa AlBayt Doha Qatar,

Walikuwa ni Jordan Henderson na Harry Kane waliofunga katika dakika sita za mwisho za kipindi cha kwanza na kuwafanya vijana wa Gareth Southgate kuwadhibiti Senegal Simba wa Teranga.

Wakati bao lao la tatu lilifungwa na Bukayo Saka naye mchezaji Jude Bellingham alihusika katika mabao yote mawili. Kwa mara ya kwanza, kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 tu alishuka chini upande wa kushoto na kumpasia Jordan Henderson ambaye aliungiza mpira kimiani na kumpita kipa wa Senegal Edouard Mendy.

Kocha wa Senegal Aliou Cisse anasema walipata nafasi lakini walishindwa kuzitumia hasa baada ya katikati ya kipindi cha kwanza, Krépin Diatta aliingilia pasi mbaya kutoka kwa Harry Maguire na krosi yake ikasababisha hati hati kwenye lango la Uingereza. Ismaila Sarr alipiga krosi ya ikagongwa mwamba wa Jordan Pickford na kutoka nje.

Jumamosi usiku kwenye uwanja huo huo Uingereza itamenyana na Ufaransa katika robo fainali ya pili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG