Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 07:28

Senegal yatinga Nusu fainali Afcon


Washabiki wa Senegalwakishangilia timu yao kupata ushindi.

Timu ya taifa ya Senegal Teranga Lions imekata tiketi  ya mwisho kuingia nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya afrika AFCON 2021 baada ya kuibwaga Equatorial Guinea kwa mabao 3-1 katika uwanja wa  Ahmadou Ahidjou mjini Yaoundé.

Timu hiyo ikiongozwa na nahodha Sadio Mane aliyerudi baada ya kutibiwa maumivu ya kichwa baada ya kugongana na golikipa wa CapeVerde Josimar Diaz au Vozinha ilifanya mashambulizi makali na kupata bao lake la kwanza katika dakika ya 28 lilowekwa nyavuni na Famara Diedhiou anayecheza soka la kulipwa katika timu ya Alanyaspor ya Uturuki.

Equatorial Guinea hawakukata tamaa na kujibu mashambulizi na hatimaye kufanikiwa kiusawazisha katika dakika ya 57 kupitia kwa Jannick Bayla anayechezea timu ya Gimnàstic de Tarragona, ya Hispania.

Senegal walionyesha umahiri wao wakisukuma mashambulizi na hatimaye kufanikiwa katika dakia ya 68 kupachika bao la pili kupitia kiungo wao hatari Cheikhou Kouyate anayechezea Crystal Palace ya Uingereza aliyeingia kipindi cha pili badala ya Papa Gueye anayechezea timu ya Olympique de Marseille.

Cheikhou akitumia urefu wake vizuri na kumruka golikipa wa Equatorial Guinea na kumalizia kwa ustadi mkubwa kuingiza mpira wavuni.

Mchezaji machachari Ismaila Sar wa Senegal anayechezea ligi ya Uingereza katika timu ya Watford alipachika bao la tatu na la mwisho na kuwaweka rasmi Senegal katika nusu fainali wakijaribu kurudia kile walichofanya 2019 kuingia katika fainali za michuano hiyo.

Sasa Senegal ili warudie historia hiyo wana kibarua cha kuwashinda Burkinafaso -Stallions siku ya Jumatano ambao watapambana nao katika nusu fainali ya kwanza, wakati ya pili kati ya Mafarao wa Mistri na Cameroon itafuata Alhamisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG