Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 10:46

Senegal wachukua kombe la Afrika kwa mara ya kwanza


Timu ya Senegal imetawazwa kuwa mabingwa wa soka barani Afrika AFCON 2021

Baada ya dakika 120 za jasho na damu timu ya taifa ya Senegal Simba wa Teranga  ilifanikiwa kutwaa kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuichapa Mafarao wa Misri  kwa mikwaju ya penati 4-2.

Hii ni baada ya kucheza dakika 90 bila kufungana ambapo Senegal watajilaumu wenyewe kwa kukosa penati mapema kabisa katika mchezo huo baada ya Sadio Mane kukosa penati iliyookolewa na golikipa wa Misri Mohamed Abou Gabal au Gabasky.

Lakini baada ya mikwaju ya penati Sadio Mane alisahihisha makosa yake na kupachika kimiani penati ya nne na ya mwisho kwa Senegal na kuweka historia ya kuchukua kombe la kwanza la Afrika kwa nchi hiyo. Senegal ilikuwa imepoteza fainali mara mbili hapo awali, zikiwemo za Kombe hilo zilizofanyika ya mwisho ikiwa nchini Misri mwaka 2019.

Fainali hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Olembe mjini Yaounde, mbele ya rais wa Cameroon Paul Biya ilikuwa ya kihistoria ikiwakutanisha nyota wawili wa ligi ya Uingereza na timu ya Liverpool Sadio Mane wa Senegal na Mohamed Salah wa Misri. Mchezaji bora wa michuano hiyo -MVP alitajwa kuwa ni Sadio Mane wa Senegal. Golikipa bora wa michuano hiyo alitajwa kuwa Eduardo Mendy wa Senegal na timu ya Chelsea.

Na kiatu cha dhahabu kilikwenda kwa mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar kwa kupachika jumla ya mabao 8.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG