Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 11:11

Sekta ya utalii Ethiopia yaporomoka


 Waandamanaji katika eneo la Oromia
Waandamanaji katika eneo la Oromia

Ethiopia ilionesha dalili za kuwa kituo maarufu cha utalii katika bara la Afrika , siyo tu kwa sababu ya kuwa na vivutio vya maeneo ya kihistoria lakini pia kutokana na usalama uliokuwepo nchini humo.

Sekta ya utalii nchini Ethiopia inataabika kutokana na matokeo ya ghasia zilizodumu kwa mwaka mmoja nan a kutangazwa kwa hali ya dharura vimesababisha kuporomoka kwa sekta hiyo.

Ethiopia ilionesha dalili za kuwa kituo maarufu cha utalii katika bara la Afrika , siyo tu kwa sababu ya kuwa na vivutio vya maeneo ya kihistoria lakini pia kutokana na usalama uliokuwepo nchini humo.

Makanisa yaliyojengwa kwa kutumia mawe kwenye mji wa Lalibela kaskazini mwa Ethiopia yanavutia maelfu ya watalii kila mwaka. Lakini tangazo la miezi sita la hali ya dharura lililotolewa wiki tatu zilizopita na serikali ya nchi hiyo linawaogopesha watalii.

Hata hivyo utalii ni chanzo chakipato kwa wakazi wengi hasa kutoka Lalibela, hivyo ikimaanisha kushuka kwa utalii nchini kunaathiri jumuiya nzima katika eneo licha ya kwamba Lalibela haijaathiriwa na maandamano na migomo . waandamanaji wa Oromo na Amahar waliingia mitaani kupinga mzozo wa ardhi baina yake na serikali.

XS
SM
MD
LG