Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:57

Scotland yapiga kura kutaka kujitenga ama la


Wapiga kura kituoni wakisubiri kupiga kura ya Ndio au Hapana huko Edinburgh, Scotland September 18, 2014.
Wapiga kura kituoni wakisubiri kupiga kura ya Ndio au Hapana huko Edinburgh, Scotland September 18, 2014.

Upigaji kura unaendelea kote Scotland kwa kura ya maoni ya kihistoria ambayo itaamua kama nchi hiyo inaondoka kwenye muungano wake wa miaka 307 na Uingereza na kuwa taifa huru.

Watu waliojitokeza katika kura ya maoni wanatarajiwa kuwa wengi kwa sababu zaidi ya watu milioni 4 na laki mbili walijiandikisha kupiga kura ambapo asilimia 97 ya watu hao wanastahili kufanya hivyo.

Wananchi wanapiga kura kwenye vituo 2,600 vya kupiga kura vilivyoko nchi nzima kwa kuchagua neno “Ndio” au “Hapana” kwenye swali la kura ya maoni linalouliza kwamba “Ni vyema Scotland iwe taifa huru?”.

Maoni ya karibuni yanawaweka waungaji mkono wa umoja huo mbele kwa asilimia pointi 4 hadi 5.

Upande unaopinga kujitenga kwa umoja huo unasihi kwamba kura ya “Ndio” itaharibu uchumi wa Scotland na kuvuruga maisha ya kila mtu kama ushirika wa Uingereza ulioundwa mwaka 1707 unavunjika.

XS
SM
MD
LG