Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:09

Saudia yasema itaendeleza sera zake thabiti za mafuta kimataifa


Kampuni ya mafuta ya Aramco inayomilikiwa na serikali.
Kampuni ya mafuta ya Aramco inayomilikiwa na serikali.

Saudi Arabia inasema itaendelea na jukumu lake kama muuzaji mkubwa wa mafuta nje ya nchi duniani hata kama inaangalia kuendeleza vyanzo vingine vya nishati wakati bei za mafuta ulimwenguni zikishuka.

Waziri mpya wa nishati, khalid al-Falih, alisema Saudi Arabia itaendeleza sera thabiti za mafuta na kusimamia jukumu lake katika masoko ya kimataifa ya nishati kama msambazaji mkubwa duniani anayeaminika wa nishati.

Alisema Saudi Arabia ina nia ya dhati kukidhi mahitaji yaliyopo na ya ziada ya hydrocarbon kufikia uwezo endelevu wa juu zaidi.

Katika mabadiliko ya serikali hapo jumamosi, Falih, mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta ya Aramko inayomilikiwa na serikali aliteuliwa kuwa mkuu mpya wa wizara ya nishati, viwanda na rasilimali za asili katika juhudi za kuubadili uchumi wa ufalme huo ambao unategemea mafuta. Anachukua nafasi ya waziri wa muda mrefu wa mafuta nchini humo, Ali al-Naimi, ambaye alifukuzwa katika wadhifa aliokuwa akiushikilia tangu mwaka 1995.

Taasisi ya nchi zinazouza mafuta nje inasema kwamba Saudi Arabia inauza nje mafuta ya zaidi ya mapipa milioni saba ya mafuta kwa siku na ina asilimia 18 ya akiba ya mafuta duniani.

Lakini mapato yake ya mafuta na gesi ni nusu ya uchumi wa Saudi Arabia na asilimia 85 ya mapato yake ya mauzo yake ya nje yamepungua kwa sababu ya kushuka kwa bei za mafuta duniani kulikosababishwa na kujaa kupita kiasi kwa mafuta kwenye soko la ulimwengu.

Kampuni ya mafuta ya Aramco iliyopo Shaybah, Saudi Arabia (file photo).
Kampuni ya mafuta ya Aramco iliyopo Shaybah, Saudi Arabia (file photo).

Saudi Arabia imekuwa ikihusika kwa kuongezeka baadhi ya mafuta ghafi kwenye soko la ulimwengu ikikataa kupunguza uzalishaji wake wa mafuta hata pale ambapo Marekani inazalisha mafuta zaidi inayohitaji kupitia utumiaji wa utaratibu wa kuchuja makapi katika uchimbaji mafuta kwa njia ya kiteknolojia chini ya ardhi ambao awali haukuweza kufikiwa.

Huku mapato ya mafuta yakishuka tangu kati kati ya mwaka 2014, Saudi Arabia ilikuwa na nakisi ya bajeti ya dola bilioni 100 mwaka jana na inabashiri upungufu mwingine wa dola bilioni 87 kwa mwaka huu wa 2016.

XS
SM
MD
LG