Hata hivyo mataifa hayo yanaonekana kutofautiana ifikapo kwenye suala la elimu, au kufanya kazi kwa wanawake. Saudi Arabia ambako hadi miaka ya karibuni wanawake walikuwa wamenyimwa haki nyingi za kijamii, idadi ya wanawake wanaofanya kazi sasa imefikia asilimia 37, kulingana na takwimu za serikali na pia kutoka kwa maafisa wa Marekani.
Kwenye sekta ya teknolojia, idadi ya wanawake wa Saudi Arabia imeongezeka kiasi kwamba balozi wa Marekani nchini humo Michael Ratney hivi karibuni kwenye hotuba yake yenye ucheshi, alisema kwamba kitovu cha teknolojia hapa Marekani cha Silicon Valley kinahitaji kuiga mfano wa Saudi Arabia.
Aghanistan kwa upande wake imeshuhudia kuminywa kwa haki za kimsingi za wanawake chini ya utawala wa Taliban, ambapo hawaruhusiwi kuhudhuria masomo au hata kufanya kazi.
Forum