Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:04

Saratani ya matiti yaongezeka Cameroon


Mfanyakazi wa afya mjini Yaounde Cameroon
Mfanyakazi wa afya mjini Yaounde Cameroon

 Wanaharakati wa afya nchini Cameroon mwezi huu wamekuwa wakitembelea nyumba za watu, mashamba pamoja na masoko wakati wakihamasisha wanawake kufanya  vipimo vya bure vya saratani  ya matiti. 

Taifa hilo la kati mwa Afrika limeshuhudia ongezeko kubwa la saratani ya matiti miongoni mwa wanawake katika kipindi cha mwaka mmoja uliyopita kwa kuwa wengi walichelewa kufanya vipomo kwa wakati kutokana na janga la corona.

Wanaharakati hao ambao wengi ni wanawake wakekuwa wakitembelea vitongoji tofauti vya Yaounde wakati wakirai wakazi kwenda kwenye hospitali ili kufanyiwa vipimo. Kila kundi lina takriban watu darzeni moja wakiwemo wataalamu wa afya, wawakilishi wa mashirika ya kiafya, wagonjwa wa saratani pamoja na familia zao.

Miongoni mwa watu wanaoshiriki kwenye zoezi hilo ni Amin Ruth Tabi mwenye umri wa miaka 24 kutoka shirika lisilo la kiserikali la Noela Lyonga. Hivi ndivyo anavyosema.

Kila mwanamke anahitaji kufanya vipomo vya saratani ya matiti siku 7 hadi 10 baada ya kumaliza siku zake za hedhi, ili kuona iwapo wana uvimbe, rangi tofauti au hata maji yanayotoka kwenye matiti. Saratani ya matiti inaweza kuponywa iwapo itaghunduliwa kwa wakati.”

Wizara ya afya ya Cameroon imesema kwamba kufuatia kampeni hiyo, maelfu ya wanawake wamejitokeza kufanyiwa vipimo kutoka kwenye takriban miji 11 ikiwemo Yaounde na Douala pamoja na miji ya magharibi ya Kumba, Buea, Limbe na Bamenda Kumbo.

Shirika la wagonjwa wa saratani nchini Cameroon linasema kwamba wengi wao hupitia hali tofauti za unyanyapaa. Baadhi ya watu wakiwemo wanafamilia wanaamini kwamba kuugua saratani ni adhabu ya aina fulani. Shirika hilo linasema kwamba mara nyingi wagonjwa wanatengwa kutokana na kutokuwa na ufahamu wa kutosha au matatizo ya kifedha.

Wizara ya afya inasema kwamba vipimo vya mapema kupitia vifaa maalum vinasaidia katika kuanza matibabu mapema na kwa hivyo kuzuia idadi ya vifo. Ripoti zinasema kwamba mwaka wa 2019, wagonjwa 3,000 kati ya 5,000 waliopatikana kuwa na saratani walikufa. Mwaka uliyopita wa 2020, kulikuwa na wagonjwa 7,000 ambapo 5,000 miongoni mwao walikufa.

XS
SM
MD
LG