Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 16:25

Samsung yasitisha kabisa utengenezaji wa Galaxy Note7


Samsung Gadgets Galaxy Note7
Samsung Gadgets Galaxy Note7

Kampuni kubwa ya vifaa vya elektronki ya Samsung iliyoi na makao yake makuu Korea Kusini, ilisema siku ya Jumanne kuwa haitatengeneza tena simu aina ya Galaxy Note 7 kutokana na matatizo yaliyojitokeza kufuatia ripoti kadhaa kote ulimwenguni kuhusu kupata joto sana kwa simu hiyo. L

Kampuni hiyo ilitangaza kufunga kabisa utengenezaji kwa maslahi ya usalama wa mnunuzi. Samsung awali ilitangaza kwamba inasitisha mauzo yote ya galaxt note 7 kote ulimwenguni na kuwashauri wateja wake kuacha haraka kutumia kifaa hicho.

Bango linaloonyesha nembo ya kampuni ya Samsung
Bango linaloonyesha nembo ya kampuni ya Samsung

Samsung imepata hasara ya asilimia 8 katika hisa zake katika soko la hisa wakati wa kufunguliwa kwa biashara hivi leo. Makampuni kadhaa makubwa ya simu za mkononi ikiwemo kampuni ya AT & T yenye makao yake hapa marekani na ya ujerumaini ya T-Mobile kila moja imetangaza jumapili kuwa imesitisha mauzo au kubadilisha simu ya galaxy note 7.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG