Rais Salva Kirr wa Sudan Kusini ameomba wananchi wake kumsamehe makosa aliowatendea. Kirr ameasema hayo Jumatano wakati wa hotuba ya mwisho wa mwaka akiwa mbele ya kikao cha bunge.
Pia aliamuru vikosi vya Serikali kusitisha mapigano na kutaoa nafasi kwa jamii kuridhiana. “ Kwa moyo wa amani ya kitaifa, msamaha na maridhiano, nawaomba watu wa Sudan Kusini kunisameshe makosa yote niliyoyafanya” alisema Rais Kirr, akiongeza kusema kuwa taifa lake linahitaji kuwa na moyo huo na kuchukua hatua bila kupoteza muda.
Rais huyo pia alitoa wito wa kuwa na mazungumzo ya kitaifa yatakayo jumuisha washika dau kutoka sekta zote wakati ghasia zikiendelea kushuhudiwa nchini humo kwa mwaka wa tatu katika baadhi ya maeneo