Ethio Telecom inayomilikiwa na serikali ya Ethiopia hadi sasa imefurahia kuwa peke yake nchini Ethiopia, nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na watu wengi zaidi, ikikadiriwa kuwa watu milioni 118.
Safaricom Ethiopia iliwasha mtandao na huduma zake katika mji mkuu Addis Ababa siku ya Alhamisi kufuatia huduma za majaribio za mtandao huo katika miji 10, ilisema katika taarifa.
Saa chache baadaye waziri wa fedha wa Ethiopia, Ahmed Shide, alisema serikali yake iliipa kampuni hiyo leseni ya kuendesha huduma ya pesa kwa njia ya simu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Ethiopia Anwar Soussa alisema huduma hiyo ya pesa kwa njia ya simu itachukua miezi miwili hadi mitatu kutekelezwa.
Safaricom inaongoza muungano unaoingia sokoni ikiwa ni pamoja na Vodacom ya Afrika Kusini na Vodafone ya Uingereza.
Mtandao wake ulipaswa kuzinduliwa mwezi Aprili lakini ulicheleweshwa kwa sababu ya janga la corona na changamoto za vifaa.