Upatikanaji viungo

Safari za ndege zaanza tena uwanja wa JKIA Nairobi

  • Esther Githui-Ewart

Maafisa wa uwanja wa ndege wanakagua eneo lililowaka moto kwenye uwanja wa kimataifa Jomo Kenyatta, mjini Nairobi, Kenya, on Aug. 7, 2013.
Wapelelezi wanaendelea na uchunguzi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata mjini Nairobi, kufuatia moto mkubwa uloanza Jumatano alfajiri na kuteketeza jengo la mapokezi ya abiria wa kimataifa.

Wakati huo huo safari za ndege za ndani ya nchi zilianza jioni ya Jumatano kwa mujibu wa katibu wa mawasiliano Kenya bw. Ezekiel Mutua ambaye aliazungumza na Sauti ya Amerika. Anasema wanatarajia safari za ndege za Kimataifa kuanza Alhamisi asubuhi.

Bw. Mutua anasema hadi jumatano jioni wapelelezi hawakujua kilichosababisha moto huo na kueleza kwamba maafisa wa usalama na kikosi cha kupambana na ugaidi wamekuwa wakikutana siku nzima na kufanya uchunguzi wao.

Maafisa wanasema mashahidi 120 kutoka idara ya usafiri wa anga ya kenya na uhamiaji wamehojiwa. Abiria elfu 16 wameathiriwa na ajali hiyo imesababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
XS
SM
MD
LG