Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:24

Afrika kusini yaonywa juu ya uwezekano wa kushambuliwa na magaidi


Islamist State ISIS ISIL Daesh
Islamist State ISIS ISIL Daesh

Uingereza na Australia wameungana na Marekani katika kutowa onyo juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi nchini Afrika Kusini. Serikali inawahamasisha waafrika kusini wasitaharuki na mchambuzi wa juu wa masuala ya ugaidi anakubali, lakini pia anasema Afrika Kusini isibweteke.

Hadi sasa, tishio la ugaidi lililoripotiwa kwa Afrika kusini halijasababisha lolote isipokuwa mkanganyiko.

Ubalozi wa Marekani ulitowa tahadhari Jumamosi kwa kuonya kuwa wanamgambo wa Islamic State huwenda wakalenga maeneo ya maduka makubwa Afrika kusini. Uingereza na Australia nazo pia zilitowa onyo kama hilo.

Hakuna serikali ya kigeni iliyoelezea mahsusi wapi tishio hilo linatokea, japo ubalozi wa marekani ulielezea tishio hilo linatokana na habari uhakika na kuaminika.

Marekani piailitowa onyo kama hilo September mwaka jana.

Nchini haionekani kuwa na wasiwasi kuhusu tishio hilo kuwa linaweza kuwepo Afrika kusini. Wizara ya usalama wa taifa ilisubiri siku 2 baada ya onyo la marekani, kutoa taarifa ambayo kimsingi walisema watu wasitaharuki.

Waziri wa usalama wa taifa, David Mahlobo anasema bado sisi ni taifa lenye nguvu na thabiti na hakuna hatari inayoletwa na onyo hilo.

Mtaalam wa masuala ya ugaidi Jasmine Opperman anakubali kuwa Afrika kusini sio mlengwa mkuu.

Opperman anasema, hakuna ushahidi kuwa Islamic State au kundi lolote lenye msimamo mkali nchini Afrika kusini, linapanga shambulizi lolote dhidi ya maeneo ya umma au ya kitalii ambako watu hukusanyika. Kwa hiyo hatari ni ndogo.

Washirika wa Al Qaida wamelenga raia katika baadhi ya mataifa ya kiafrika ambayo yamewapinga kama vile Ivory Coast,Kenya, na Uganda. Na kundi la Boko Haram la Nigeria linalodai kuwa na uhusiano na kundi la Islamic state, limefanya mashambulizikatika nchi jirani.

Hata hivyo msemaji wa wizara ya usalama wa taifa Brian Dube anasema Afrika kusini iko mbali na viwanja hivyo vya mapambano, na pia siyo mhusika mkuu wa kimataifa katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic state.

Lakini Opperman ambaye ni mkrugenzi wa Southern Africa Operations at Terrorism reseach and Analysis Consortium, anasema hiyo haimaanisha kuwa Afrika kusini iko huru .

Anasema inakadiriwa kuwa baina ya waafrika kusini 20 hadi 80 wamejiunga na kundi la Islamic State. Wengi wao kama walimu, na wasimamizi na sio kama wapiganaji. Anasema taarifa alaozipata haionyeshi ishara kuwa kuna vikundi vilivyoundwa au mashambuzlizi yalopangwa nchini Afrika kusini

Hata hivyo si Marekani, Uingereza wala Australia inawashauri raia wake kuacha kusafiri kwenda Afrika kusini.

XS
SM
MD
LG