Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 14:06

El Nino yatishia kilimo Afrika Kusini


shamba la mahindi karibu na Vanderbijlpark nje wa mji wa Johannesburg, Africa Kusini , Oct. 1, 2015.
shamba la mahindi karibu na Vanderbijlpark nje wa mji wa Johannesburg, Africa Kusini , Oct. 1, 2015.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema El Nino itapelekea ukame na mafuriko katika sehemu za Afrika Mashariki na kusini mwaka huu.

Ukame mbaya pamoja na joto kali linaikumba sekta ya kilimo ya Africa Kusini, pale eneo hilo linapojianda kupambana Zaidi na athari za matokeo ya El Nino.

Wataalam wa hali ya hewa wanaelezea ukame huo kuwa mbaya Zaidi kuwahi kuathiri Afrika kusini katika kipindi cha miaka 23. Wataalam wanalaumu El Nino, mfumo wa hali ya hewa duniani ambao unathiri vipimo vya joto katika bahari kwenye maeneo ya equatorial ya pacific kila baada ya miaka kadhaa.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema El Nino itapelekea ukame na mafuriko katika sehemu za Afrika Mashariki na kusini mwaka huu.

Afrika kusini tayari imeshapata ukosefu wa mvua katika mismu miwli. Na Francois Engelbrecht, mtafiti wa baraza la sayansi na utafiti wa viwanda CSIR inasema mwaka huu hali bado ni tete.

Engelbrecht anasema tumeona rekodi ya hali ya joto ikivunjwa mwaka huu, na El Nino kawaida huhusishwa na mvua haba katika msimu wa kati wa hali ya joto. Sasa bado haijakuja. Kipindi hicho ni baina ya mwezi December hadi Februari.

Kutokana na hali hiyo, wakulima sasa wanatarajia kupanda mbegu zao la mahindi katika hekari takriban 2.5 millioni, hiyo ikiwa ni upungufu wa asli mia 3.8 kutoka mwaka jana. Kupunguka kwa mazao na wanyama, kadhalika, kiwango cha riba katika mikopo ya benki, kutasababisha wakulima kupoteza takriban dola millioni mia 7. Mchumi wa masuala ya kilimo Wandile Sihlobo anasema, mzozo huo utaawaathiri wateja.

Sihlobo anasema,tayari athari ipo. Unatazamia bei za mahindi sasa. Ziko asli mia 67 zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana, na mahindi ya rangi ya manjano yako asli mia 45 juu Zaidi kuliko yalivyokuwa mwaka jana. Kwa hiyo, hii yote itaanza kuvuja na watu wataanza kuona bei za bidhaa zimepanda.

Serikali ya Afrika kusini imetangaza majimbo yote ya Kwazulu Natal na Free State kama maeneo yalokumbwa na janga, kutokana na upungufu wa maji. Maafisa wanatarajia kutangaza maeneo mengine mawili kama maeneo yalokumbwa na janga la kilimo hivi karibuni, nayo ni majimbo ya Limpopo na Mpumalanga. Tangazo hilo linaipataia nguvu serikali ya kitaifa kuingilia kati.

Serikali imetenga kando takriban dola millioni 25 kukabiliana na upungufu wa maji. Hii ni pamoja na kutuma magari ya mapipa ya maji katika jamii ziloathirika na kadhalika pia watachimba visima.



XS
SM
MD
LG