Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 13:23

Agathon Rwasa ajitokeza Bujumbura kutoka mafichoni


Agathon Rwasa akiwasili kutoka mafichoni na kuzungumza na waandishi habari
Agathon Rwasa akiwasili kutoka mafichoni na kuzungumza na waandishi habari
Kiongozi mkuu wa upinzani na kiongozi wa wa zamani wa waasi wa kundi la FNL, nchini Burundi Agathon Rwasa ajitiokeza hadharani kwa mara ya kwanza Jumanne mjini Bujumbura.

Kiongozi huyo alizuiliwa na vikosi vya usalama kukutana na wafuasi wake katika ukumbi ulopangwa kufanyika mkutano wake na kulazimika kuelekea nyumbani kwake.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Wakuu wa usalama wamedai kwamba hakuwa na kibali kinachohitajika kuanda mkutano kama huo katika ukumbi huo. Kutokana na hatua hiyo wafuasi wa Bw. Rwasa walowasili kwa miguu kutoka pembe zote za Bujumbura waliandamana na kiongozi wao hadi nyumbani kwake.

Bw Rwasa anaechukuliwa kama kiongozi mkuu wa upinzani nchini Burundi ni mpinzani mkuu wa Rais Pierre Nkurunziza aliyeko madarakani tangu mwaka 2005, aliyekimbilia mafichoni mwaka 2010 baada ya uchaguzi mkuu ambao alidai uligubikwa na wizi na kasoro chungu nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake karibu na ikulu ya rais, kiongozi wa chama cha FNL amesema hajawahi kutoka nje ya mipaka ya nchi tangu kukimbia kwake miaka mitatu iliyopita, na atagombania kiti cha rais 2015.

Bw. Rwasa alitoa wito kwa wote walonyimwa haki na amani kuungana nae na chama chake FNL kuleta mabadiliko muhimu yanayohitajika katika utawala wa Burundi.
XS
SM
MD
LG