Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:46

Rwanda: Mwanamke mmoja akabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela kwa kuvaa 'mavazi ya aibu'


Waziri wa zamani wa sheria Johnston Busingye, picha ya AFP
Waziri wa zamani wa sheria Johnston Busingye, picha ya AFP

Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikamatwa nchini Rwanda kwa shutuma za kuvaa mavazi ya aibu anakabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela, waendesha mashtaka wamesema Alhamisi.

Liliane Mugabekazi alikamatwa tarehe 7 Agosti baada ya kuhudhuria tamasha la mwanamuziki maarufu wa Ufaransa Tayc siku nane kabla, akiwa amevalia mavazi yanayoonyesha mwili wake.

“Alihudhuria tamasha hilo akiwa amevalia nguo zinazoonyesha sehemu zake za siri, nguo ambazo tunaziita za aibu,” waendesha mashtaka wamesema, wakimtuhumu kufanya uhalifu mkubwa.

“Ni kwa sababu hizi nzito tunaiomba mahakama kumweka rumande Mugabekazi kwa siku 30.”

Msemaji wa mwendesha mashtaka, Faustin Nkusi, ameiambia AFP “Anashukiwa kufanya tendo la aibu hadharani,” akiongeza kuwa mahakama itatangaza Jumanne ijayo ikiwa ataachiliwa kwa dhamana.

Habari za kukamatwa kwa mwanamke huyo zilizusha hasira miongoni mwa baadhi ya Wanyarwanda, lakini maafisa wa serikali akiwemo waziri wa zamani wa sheria Johnston Busingye waliunga mkono hatua hiyo.

Katika mahojiano ya televisheni wiki iliyopita, msemaji wa polisi John Kabera alikemea kile alichokiita “ukosefu wa maadili na adabu” miongoni mwa vijana.

XS
SM
MD
LG