Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 07:51

Serikali ya Rwanda yapinga shutuma za mauaji kwa raia wake


Serikali ya Rwanda yapinga shutuma za mauaji kwa raia wake

Serikali ya Rwanda inasema inapinga vikali shutuma za polisi wa Uingereza kwamba inataka kuwauwa waasi wawili raia wa Rwanda wanaoishi london.

Taarifa ya Rwanda inasema tuhuma hizo si sahihi na za uongo, ikisema kwamba polisi hawana ushahidi wowote wa hilo. Taarifa inasema serikali ya Rwanda haijawahi kutumia ghasia dhidi ya raia wake au kuwatishia maisha yao, popote pale walipo.

Gazeti la Times of London liliripoti wiki iliyopita kwamba polisi wa London walituma barua kuwaonya raia hao wawili wa Rwanda, afisa wa zamani wa jeshi, Jonathan Musonera na Rene Mugenzi, ambaye anaendesha taasisi ya utafiti. Wote ni wakosoaji wakubwa wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Shutuma katika barua hizo zinasema kwamba serikali ya Rwanda imeweka vitisho kwa maisha yao na inawasihi watu hao kuchukua tahadhari za ziada. Polisi wa London hawajathibitisha ripoti za gazeti la Times of London.

XS
SM
MD
LG