Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:38

Russia yazidisha mashambulizi dhidi ya miji mingi ya Ukraine

Sehemu iliyoharibiwa ya monasteri ya Kikristo ya Othodox- The Holy Dormition Svyatogorsk Lavra kando ya mto Siverskyi Donets inaonekana, wakati uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine ukiendelea, katika eneo la mashariki la Donbas la Sviatohirs'k, Ukraine, Oktoba 31, 2022.(REUTERS)

Russia ilizidisha mashambulizi yake dhidi ya miji mingi ya Ukraine Jumatatu, ikilenga miundombinu muhimu na kuondoa usambazaji wa umeme na maji huko Kyiv na mikoa mingine. Mashambulizi hayo yametokea siku moja baada ya Russia  kudai kuwa Ukraine ilishambulia meli zake zilizoko Black Sea.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema mashambulizi katika mji mkuu yalikata umeme na usambazaji wa maji katika baadhi ya maeneo ya jiji, na kuacha zaidi ya asilimia 80 ya wakaazi wake bila maji ya bomba. Kufikia usiku, idadi hiyo ilipungua hadi asilimia 40.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alilaani mashambulizi hayo, akiandika:

"Makombora mengine ya Russia yamepiga miundombinu muhimu ya Ukraine. Badala ya kupigana kwenye uwanja wa vita, Russia inapigana na raia. Usihalalishe mashambulizi haya kwa kuyaita 'majibu.' Russia inafanya hivi kwa sababu bado ina makombora na nia ya kuwaua raia wa Ukraine."

XS
SM
MD
LG