Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 14:01

Russia yatupilia mbali mpango wa amani wa Rais Zelenskiy wa kuitaka kuondoa wanajeshi wake


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akishiriki mkutano wa viongozi wa G7 kwa njia ya mtandao, Disemba 12, 2022.

Russia Jumanne imetupilia mbali mpango wa amani wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ambao unapendekeza kuondolewa kwa wanajeshi wa Russia, ikisema Kyiv inahitaji kukubali ukweli kuhusu maeneo yanayokaliwa na Russia.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema ukweli huo ni kuhusu maeneo manne ya Ukraine ambayo ilitangaza mwezi Septemba kuwa maeneo huru chini ya udhibiti wa Russia, hatua ambayo Umoja wa Mataifa ulilaani kuwa si halali.

Peskov alikuwa akijibu kuhusu ombi la rais Zelenskiy kwa viongozi wa kundi la G7 jana Jumatatu kupewa vifaa zaidi vya kijeshi, msaada wa kifedha na uthabiti wa nishati, na kuunga mkono suluhisho la amani ambalo litaanza kwa Russia kuondoa wanajeshi wake nchini Ukraine, kuanzia Krismasi hii.

Peskov amesema “Kuna hatua tatu kuelekea kumaliza uhasama”, akiongeza kuwa Ukraine inahitaji kuzingatia hali halisi inayoendelea wakati huu.

Amesema “Ukweli huu unaonyesha kuwa maeneo mapya yamepatikana ndani ya shirikisho la Russia, na yalipatikana kama matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika katika maeneo hayo.”

Hilo likizingatiwa, hakuna budi kwa Russia kuanza kuondoa

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG