Serikali ya Russia imeripotiwa kwamba inapanga kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha ya kiingereza.
Hatua hiyo inatokana na kile Russia inataja kama hatua zisizo za kirafiki, zinazochukuliwa na serikali za nje dhidi ya Russia.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Maria Zakharova amesema kwamba Russia inatayarisha hatua itakazochukua hivi karibuni dhidi ya vyombo hivyo vya habari.