Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 18:54

Russia yasema Ukraine imefanya mashambulizi mpaka Moscow


Maafisa wa Russia, wamesema Ukraine imeanzisha mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani mapema Jumapili, na kulenga maeneo kadhaa ya Russia, vikiwemo vinu vya umeme na vya kusafisha mafuta vya Moscow na mji wa karibu wa Tver.

Russia imesema wanajeshi wa kikosi cha anga walinasa na kuharibu ndege 158 za Ukraine, zikiwemo mbili juu ya Moscow na tisa katika eneo jirani.

Ndege zisizo na rubani 46 zilinaswa juu ya Kursk, ambayo imeshuhudia kuongezeka kwa mashughuli ya Ukraine. Meya wa Moscow Sergei Sobyanin, ameripoti kuwa mabaki yaliyoanguka kutoka kwenye ndege mbili zisizo na rubani yalisababisha moto kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta.

Alieleza kuwa moto huo ulikuwa katika chumba tofauti cha kiufundi kwenye mtambo huo, lakini shughuli hazikuathiriwa. Shirika la habari la serikali TASS baadaye lilinukuu idara za huduma za dharura ikisema moto huo umezimwa.

Forum

XS
SM
MD
LG